Dedication to all friends.
For somehow life has treated us so BUSY that we don't see each other or not have time 2 chat.
Friend
Kimya chako nakiwaza,Najua umekumbatwa.
Nabaki najiuliza, Jinsi nnavyo fukutwa.
Ni lipi lakutatiza, Au wataka fuatwa.
Hali yako nauliza, Wajua sitaki pitwa
Wanionyesha simanzi,Kila nikifikiria
Wangu rafiki kipenzi,Kimya amejikalia
Hebu nifungue tenzi,Nakuwaza nasinzia
Rafiki hujambo kipenzi,Au kuna kitu chasumbua
Reply:
Siwezisema nimebwana, ila maisha kama fukuto.
Kwenda mawio mpaka macheo, mvua, baridi, joto.
Kila siku twazipigania, ahadi moyoni kukamilisha.
Hamna kinachosumbua, nashukuru kwa hali nitakia
Mitihani, kazi, famalia, rafiki ni sehemu yetu mwili
Vyote kuvipigania, kugawa wakati hupatia upendeleo.
Kipaombele cha kila mtu hujua mwenyewe, lipi lianze
Yote na umuhimu wake, tunaomba mola atupe uzima.
Friend
Zimepowa zangu nyoyo,Kauli yako kusikia.
Yamenishia mayoyo,Baridi sasa nasikia
Umefurahika moyo, Kwavile kunandikia.
Pole kwa yakusibuyo,Mungu atakutangulia
Friday, January 22, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment