Friday, January 22, 2010
Mambo dada sijui nimekufananisha.
Nadhani unamjua kijana anaitwa..
Yule mvulana ni wangu tena ni mali yangu. (1)
Nani anajua majina wavulana wako wengi,
Ila kama unamzungumzia yule kijana basi umepotea.
Kwangu amefika na wala sijui kama anamwingine. (2)
Tusijegombana bure na urafiki ukatuisha.
Tangulini awe wako mwenyewe aishia kwangu
Kijana mahibibi tena mali yangu (1)
Sumu siniwekee ukamchukua aliye wangu
tusijegombana bure na urafiki ukatuisha
Vitu vyote vya thamani kwangu huniletea
Wala sijaomba, mwenyewe huja kujitetea
Sehemu mbalimbali tutakuja tembea (2)
Tusijegombana bure na urafiki ukatuisha
Siwezi amini uloyatamka mdomoni
nilidhani mimi nawe kama samaki na maji (1)
iweje leo utembee na wako shemeji
tusije gombana bure urafiki ukatuisha
Aliponiita baby hakusema tuko wengi
Mimi sikujua kama ana mwingine pembeni (2)
Mimi sina kosa dada naziomba samahani
Tusijegombana na urafiki ukatuisha.
Tusigombana bure na urafiki ukatuisha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment