Social Icons

Pages

Friday, January 22, 2010

POEM ~ Dua Yangu

Dua yangu~ (My prayers)


Alhamdhulillahi jamani nnafurahia,
Bila shaka wakati sasa umewadia,
Hivi wasaa kidogo tu ndo umesalia,
Dua yangu Rabana tafadhali sikia.

Mdogo, mdogo siku poa nimezifikia,
Shukran Mola kwa uzima ulonipatia,
Baraka nazo n nyingi ulzonitunukia,
Dua yangu mie Mola nakusihi, Sikia.

Naomba Dua, natumai Jalali yakufikia,
La kwanza uwepo wako katika hii njia,
Uwe nami wakti wote kwenye hii dunia,
Dua yangu ewe Muumba jamani sikia.

Mahasidi Uhasama wao wakinizidishia,
Wanafki wenyechuki watakaponzushia,
Chini ya mbawa zako upate kunifunikia,
Dua yangu Rabuka nakulilia upate isikia.

Pili siwasahau jamaa na yangu familia,
Ma' baba dadazangu na wangu malikia,
Tutunze sote na marafiki wetu nao pia,
Dua yangu... Rahimu naomba utaisikia.

Tuepushe yule mwovu, najua ywasikia,
Mpaka siku ya ile mwisho tutakapoifikia,
Hapo kiama pale Mbiu yako itakapolia,
Dua yangu...Bwana nifurahike ulinisikia.

Milango yako ya Lulu utakapotufungulia,
Na Matano mwenzangu tupate furahikia,
Kwenye mji wa Dhahabu tupate jumuikia,
Dua yangu Jalali nikushukuru kwa kusikia.

Original by Mathew Ngao, one of my best friend & teachers of Swahili poems. There is more to this guy and i would like to suscribe his skills to Swahili poems to people. This is one of his poem which has touched me a lot but there are many others poems from this guy, if any wonderings, search for him personal.

English version of My prayers

{Thank You}

DEARGOD: I want to thank You for what you have already done. I am not going to wait until I see results or receive rewards; I will keep on thanking you because there is more from you than what we see in our human eyes. Because of that, u will keep on being ''the only one in my life.''

No comments: